​​

Press Release : | Ikirundi, English, Français

Majaji wa Mahakama ya ICC wanaruhusu rasmi uanizishaji wa upelelezi katika Jamhuri ya Burundi

ICC-CPI-20171109-PR1342 


Leo, tarehe 9 Novemba 2017, Chumba cha Utangulizi III cha Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (« Mahakama ya ICC «  au « Mahakama ») kinachoundwa na majaji Chang-ho Chung (jaji Rais), Antoine Kesia-Mbe Mindua na Raul Pangalangan, kiliweka hati rasmi ya hadharani iliyofutwa maneno na ambayo inamhurusu Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya ICC kuuanzisha upelelezi kuhusu makosa ya jinai yaliyo  chini ya mamlaka ya Mahakama, yanayodaiwa kuwa yalitendwa Burundi au yalitendwa na raia wa Burundi wanaoishi inje ya nchi yao, tangu tarehe 26 Aprili 2015 hadi tarehe 26 Oktoba 2017. Mwendesha Mashtaka anaruhusiwa kupanua upelelezi hata kuhusu makosa ya jinai yaliyotendwa kabla ya tarehe 26 Aprili 2015 au yale yaliyotendwa baada ya tarehe 26 Oktoba 2017, ilimradi masharti fulani ya kisheria yaheshimishwe.

Kwanza, Chumba cha Utangulizi III kilitoa uamzi wake wa siri tarehe 25 Oktoba 2017. Baada ya kumuomba Mwendesha Mashtaka habari za ziada, Chumba kilikubali kwa namna ya pekee ya kwamba utaratibu unaohusu ruhusa ya uanzishaji wa upelelezi, unaweza kwendeshwa kwa siri, kwa kumshirikisha tuu Mwendesha mashtaka.  Hiyo ni namna ya kunusuru hatari zinazoweza kumba  maisha na maslahi ya waathiriwa na wale wanaotarajiwa kuwa  mashahidi. Pia, na kwa namna ya kipekee, Chumba kilimruhusu Mwendesha Mashtaka kusukuma  baada ya siku 10 za kazi kabla ya kuzijulisha   nchi zinazohusika na makosa ya jinai yanoyodaiwa, taarifa ya uanzishaji wa upelelezi, ili zijitayarishe na kutekeleza mipango ya usalama kwa ajili ya kuzuia hatari zinazoweza kuwakumba waathiriwa na mashahidi wanaotarajiwa.  

Chumba cha Utangulizi kilibaini ya kwamba Mahakama ina uwezo wa kisheria kuhusu makosa ya jinai ambayo yanadaiwa kutendwa wakati Burundi ilikuwa bado nchi mojawapo ya zile zinazounda Mahakama chini ya Mkataba wa Roma. Burundi ilikuwa kweli mmoja kati ya nchi zinazounda Mahakama tangu Mkataba ulianza kutumika na kuhusika na nchi hii (tarehe 1 Desemba 2004) hadi mwisho wa mwaka ambayo Burundi iliomba kujitoa  (tarehe 26 Oktoba 2017).  Kujitoa kwake kulikubaliwa tarehe 27 Oktoba 2017. Kwa hiyo, Mahakama inabaki na uwezo wa kisheria kuhusu kosa lolote la jinai lililo chini ya mamlaka yake ikiwa kama lilitendwa hadi tarehe 26 Oktoba 2017. Inamaanisha ya kwamba Mahakama inaweza kutumia uwezo wake wa kisheria hata baada ya Burundi kujiondoa  na kutoka kwake rasmi, ikiwa kama upelelezi au mashtaka yanahusu makosa ya jina ambayo yanadaiwa kutendwa wakati nchi hii ilikuwa mmoja kati ya nchi zinazounda Mahakama chini ya Mkataba wa Roma. Isitoshe, Burundi inaombwa kushirikiana na Mahakama katika upelelezi huu, kwa sababu kuanzisha upelelezi iliruhusiwa tarehe 25 Oktoba 2017, kabla ya tarehe ya kutoka rasmi kwa nshi hii. Wajibu wa kushirikiana unahitajika wakati wote  upelelezi utakapoendeshwa, na utatekelezwa kwa ajili ya utaratibu wote unaohusiana na upelelezi huu. Burundi ilikubali mapashwa haya wakati ilisaini rasmi Mkataba wa Roma.

Chumba cha Utangulizi III kiliamua ya kwamba alama za ushuhuda ambazo Mwendesha Mashtaka alileta pamoja  na mawasiliano yake na waathiriwa, zinaonesha kuwa kuna sababu za kutosha kwa kuanzisha upelelezi kuhusu makosa ya jinai dhidi ya ubinadhamu yanayodaiwa kuwa yalitendwa na raia wa Burundi  tangu tarehe 26 Aprili 2015 katika nshi ya Burundi na, katika hali zingine, inje ya nchi ; ni kusema : a) mauwaji na kujaribu kuuwa ; b) kufunga gerezani au kunyima kwa kiwango kikubwa uhuru wa mtu ; c) mateso ; d) ubakaji, e) upotezaji wa watu kwa kulazimisha ; f) utesaji. Iliripotiwa ya kwamba takriban zaidi ya watu 1,200 waliuwawa, maelfu ya watu  waliwekwa kizuizini kinyume na sheria na maelfu ya watu wengine waliteswa ; na mamia ya watu walilazimishwa kupotea. Matendo ya ukatili yanadaiwa  kutendeka na kulazimisha watu 413,490 kuhamishwa kati ya mwezi wa nne na mwezi wa tano 2017.

Madai ni kwamba makosa yale ya jinai yalitendwa na wafanyakazi wa Serkali na makundi mengine ambayo yanatekeleza siasa ya Serkali, kati yao kuna Polisi ya Burundi, Kikosi cha upelelezi na tawi la jeshi la Burundi waliofanya kazi wakiheshimisha nguzo za utawala zenye muundo moja, pamoja na wanamemba wa Imbonerakure, Kikosi cya vijana ambao wanaunga mkono chama chama kinachotawala.

Mwendeesha mashataka wa ICC hatakiwe kuchunguza tu matendo na makosa ya jinai kama vile inaandikwa kwatika azimio la majaji, lakini anaweza, kwa msingi wa  alama za ushuhuda, kupanua upelelezi wake kwa makosa mengine ya jinai dhidi ya ubinadamu au makosa mengine yaliyo chini ya uwezo wa kisheria ya Mahakama   (ni kusema mauaji ya kimbari au makosa ya jinai ya kivita), ilimradi afanye kazi yake bila kutambuka mipaka ya ruhusa alipewa kuhusu upelelezi.

Kwa kumalizia, Chumba kilitambua ya kuwa, kufuatana na habari zilizoko, wakubwa wa Serkali ya Burundi hawakufanya kitu chochote kuhusu maswala ambayo yanasababisha hali ya leo nchini. Hata kama kamati tatu za upelelezi ziliundwa na taratibu kadhaa zilianzishwa mbele ya makakama za kitaifa, Chumba kiliazimu ya kwamba hatua zile hazikutosha au hazikuhusu  watu au makosa ya jinai ambayo yatacungunzwa na upelelezi wa ICC. Kwa hiyo, hakuna kugongana kati ya Mahakama na Burundi kwa mujibu wa uwezo wake wa kisheria.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka itakusanya alama za ushuhuda ambazo zinahitajika kutokea vyanzo mbalimbali vya kuaminika, kwa namna ya huru, kwa adili, na bila upendeleo. Upelelezi utachukua muda unaohitajika kwa kuzipata zile alama za ushuhuda. Kama Mwendesha Mashtaka anapata alama za kutosha za kuonesha ya kwamba kuna watu kadhaa ambao wana dhima ya kosa la jinai, ataomba majaji wa Chumba cha Utangulizi III watoe samansi au hati za kuwakamata wale watu.

Toleo la umma ambalo maneno yalifutwa la " Uamuzi kwa mujibu wa Ibara 15 ya Mkataba wa Roma kuhusu kuruhusu upelelezi katika Jamhuri ya Burundi »

kufahamishwa : utafsiri wa Kifaransa wa uamuzi huu utakuwa tayari kamili tarehe 1 Desemba 2017

Hati ya maulizo –Majibu

Mpango kupitia vielelezo vya kusikia na kuona « Ulizeni Mahakama »

YouTube (kwa kuona)

Video (MPEG-4) kwa kupakua

Audio (MPEG-3) kwa kupakua


Kuhusu habari ziada, tafadhali ulizeni Fadhi El Abdallah, Msemaji wa Mahakama na Mkurugenzi wa Kitengo cha habari kwa umma, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, nambari ya simu +31 (0)70 515-9152 au +31 (0)6 46448938, au kupitia barua pepe [email protected].

Mnaweza kufuata Shughuli za ICC kupitia mifumo ya kieletroni. Twitter, facebook, Tumblr, YouTube na Flickr.