​​

Statement : | English, Français

Taarifa ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, Fatou Bensouda, juu ya uondoaji wa Mashtaka dhidhi ya Bwana Uhuru Muigai Kenyatta

Mnamo tarehe 3 December 2014, Majaji wa Tawi la kesi cha Chumba cha V (B) wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) walikataa kuhairisha mashtaka katika kesi ya Bwana Uhuru Muigai Kenyatta. Kufuatana na hali ya ushahidi katika kesi hii, sina njia nyingine yeyote bali kuondoa mashtaka dhidhi ya Bwana Kenyatta.

Asubuhi ya leo, nimefaili tangazo ya kuondoa mashtaka dhidhi ya Bwana Kenyatta. Ninafanya hivi bila kuleta madhara kwamba nitaanza kesi mpya wakati ambapo ushahidi mwingine zaidi utakapatikana.

Hii ni wakati wa uchungu kwa mabwana, mabibi na watoto walioteswa vibaya sana katika vitisho vya ghasia ya baada ya uchaguzi na waliosubiri kwa ustamilivu karibu miaka saba kwa kuona haki imefanyika.

Nimeamua kuondoa mashtaka dhidhi ya Bwana Kenyatta baada ya kuangalia kwa makini ushahidi wote niliokuwa nao kwa wakati huu. Nimetegemea hatua hii kufuatana na ukweli maalum ya kesi hii, bila kuzingatia jambo lingine lolote. Kama vile Mwendesha Mashtaka, vitendo na maamuzi yangu vimeongozwa kwa kawaida na sheria pamoja na ushahidi.

Ijapokuwa msimamo wangu binafsi ya kuendelea na kufuata haki na kuwajibika kwa Wakenya waliokabiliwa na kunyanyaswa wakati wa ghasia iliotokea miji za Nakuru na Naivasha baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, Ninaweza tu kuendelea na kesi kama nina matarajio ya kutia hatiani katika kesi kulingana na ushahidi nilionao . Kama hakuna matarajio ya namna hiyo, basi ni wajibu wangu maulama kama vile Mwendesha Mashtaka kuondoa mashtaka dhidhi ya mshtakiwa.

Mnakumbuka ya kwamba tarehe 5 September 2014, niliomba Chumba cha Tawi la kesi kuahirisha kesi ya Bwana Kenyatta hadi Serikali ya Kenya itashirikiana kikamilifu na Ombi Mpya la taarifa ya Aprili 2014 ya Mwendesha Mashtaka. Nilieleza Chumba wakati huo kwamba ushahidi wangu ulibaki vile vile kama wakati niliomba huarishaji wa tarehe ya kesi mnamo December 2013, na kwa hivyo siku tarajia kwamba ushahidi ilikuwa ya kutosha kwa kuonyesha kwamba Bwana Kenyatta alihusiana na jukumu ya madai ya jinai zaidi ya shaka kama vile inahitajika katika kesi.

Licha biidi yangu na nia ya Timu yangu kuendelesha utaratibu wa sheria katika Kenya, kwa wakati huu, wale waliohusika na kutaka kuzuia njia za sheria, kwa sasa wanawanyima wananchi wa Kenya haki wanayo stahili.

Nimeeleza kwa wananchi wa Kenya vikwazo vikali ambayo Ofisi yangu imekabiliana nayo kuhusu uchunguzi wa Bwana Kenyatta. Hizi ni pamoja na mambo kama vile:

  • Watu wengi waliotoa ushahidi muhimu kuhusu vitendo vya Bwana Kenyatta wamefariki, wakati ule ule wengine walikuwa na hofu kuwa washahidi wa Mwendesha Mashtaka;
  • Washahidi muhimu waliotoa ushahidi kwa kesi hii walijiondoa ama walibadilisha maelezo yao, na hasa, washahidi walio hatimaye dai kwamba walisema uongo kwa Ofisi kuhusu kuwa binafsi kwa mikutano muhimu; na
  • Kutotekeleza kwa Serikali ya Kenya kumeathiri uwezo wa Mwendesha Mashataka kuchunguza kwa bidii sana mashataka  kama vile hivi karibuni ilithibitishwa na uamuzi wa Chumba.

Nimeondoa mashtaka dhidhi ya Bwana Kenyatta kwa sababu sikubali ya kwamba inawezekana kwa wakati huu, kuchunguza kikamilifu na kuweza kushtaki makosa katika kesi hii. Kuondoa mashtaka imaanishi kwamba kesi imeudumu kuachiswa. Bwana Kenyatta haja achiliwa huru na kesi inaweza anzishwa kwa aina nyingine, kama ushahidi mpya inaweza onyesha jukumu na wajibu wake.   Ofisi yangu itaendelea kupokea na kuchunguza habari itakayo toa mwanga kwa wale wenye kuwa na jukumu katika ghasia ya baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008, na nitaendelea kuthamini nini hatua zaidi tunaweza fuata halisi wakati huu kulingana na makosa ya jinai iliyofanywa kule Nakuru na Naivasha kulingana na hali ya sasa nchini Kenya.

Hata hivyo, ninataka kusema mambo machache kuhusu kushindwa kwa Serikali ya Kenya kushirikiana kikamilifu na uchunguzi wangu katika kesi hii. Kutoka wakati Mwendesha Mashtaka alitoa Ombi mpya wa tarehe 8 Aprili 2014 kwa Serikali ya Kenya, ushahidi unaoathiri kesi Serikali iliotuma haikujibu sehemu kubwa Ombi mpya ya taarifa. Kwa kifupi, maombi ya ushahidi unaoathiri kesi iliotakikana kwa Ombi mpya haikutolewa. Hii ni licha ya thibitisho ya Majaji wa ICC waliokubali waziwazi ya kwamba ombi langu mpya ilikuwa sawa, na wakakataa pingamizi la Serikali.

Wakati kama huu, ushahidi maalum wa maandishi kuhusu ghasia ya baada ya uchaguzi inaweza kupatikana tu nchini Kenya. Hata hivyo, licha ya uhakikisho ya nia yake ya kushirikiana na Mahakama, Serikali ya Kenya imekataa kufuatilia hizo hakikisho.

Hatimaye vikwazo ambazo tumevipata kwa kujaribu kupata ushirikiano unaohitajika kwa uchunguzi huu kwa sehemu kubwa, pamoja na kwa mfululizo, imechelewesha na kuzuia mkondo wa sheria kwa waathiriwa katika kesi hii. 

Kwa kumalizia, leo ni siku ya giza kwa sheria za kimataifa ya jinai. Lakini hata hivyo, ni imani yangu imara kwamba uamuzi wa leo sio neno la mwisho kwa haki na uwajibikaji kwa ualifu iliofanyika kwa wananchi wa Kenya miaka za 2007 na 2008; uhalifu ambazo zinaendelea kulilia haki.

Chanzo: Ofisi ya Mwendesha Mashtaka

Source : Office of the Prosecutor