​​

Statement : | English, Français

Taarifa ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, Fatou Bensouda, juu ya hali ya ushirikiano wa Serikali ya Kenya na uchunguzi wa Mashtaka katika kesi ya Kenyatta

Mnamo tarehe 3 December 2014, Majaji wa Tawi la kesi la Chumba cha V (B) wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wameamua ya kwamba Serikali ya Kenya walishindwa vya kutosha kushirikiana kikamilifu na uchunguzi wangu katika kesi dhidhi ya Bwana Kenyatta. Chumba kilisema, "kimeona kwamba, kwa mfululizo, mtazamo wa Serikali ya Kenya […] imepungua kiwango cha nia njema ya ushirikiano mzuri" na kwamba kushindwa hii imefikia kizingiti cha kutotekeleza kinachotakikana chini ya Mkataba wa Roma.

Kwa hivyo, katika uamuzi wake, Chumba  kimeona, "[...]  kwamba kutotekeleza kwa Serikali ya Kenya bali kumeathiri uwezo wa Mwendesha Mashtaka kuchunguza kwa bidii sana mashtaka, lakini pia hatimaye imezuia uwezo wa Chumba wa kutimiza majukumu yake chini ya Ibara 64, na hasa, kazi yake ya utafutaji ya ukweli kwa kufuatana na Ibara 69 (3) ya Mkataba." Hii ni uamuzi muhimu.

Majaji hivyo wameamua hadhi ya ushirikiano wa Serikali ya Kenya katika kesi dhidhi ya Bwana Kenyatta. Kinyume cha matangazo ya umma ya Serikali ya Kenya kwamba wamefuata kikamilifu majukumu yao kisheria katika kesi hii, uamuzi umethibitisha kwamba kwa kweli Serikali ya Kenya imevunja majukumu yake chini ya Mkataba wa Roma kwa kushindwa kushirikiana na uchunguzi wangu.

Nimeendelea kutafuta ili nipate ushirikiano Ofisi yangu ilihitaji kutoka Serikali ya Kenya katika kesi hii ili nitekeleze mamlaka yangu. Ushahidi muhimu wa maandishi kuhusu ghasia ya baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008, pamoja na habari za mwenendo ya mshtakiwa, inaweza kupatikana tu nchini Kenya na inaweza tu kupatikana kwa Mwendesha Mashtaka na msaada wa Serikali ya Kenya. Msaada huu muhimu hatimaye haukutolewa, kama vile ilithibitishwa na uamuzi wa hivi karibuni wa Chumba.

Na zaidi ya  kushindwa kwa Serikali ya Kenya, Ofisi yangu imepata vikwazo vingine vikubwa, ambaye vimekumbana na uwezo wangu wa kuchunguza kabisa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008 na hatimaye imezuia uchunguzi katika kesi hii. Hizi ni pamoja na: 

  • Mkondo wa taarifa za uongo kabisa thabiti na yasiyokoma  kwa vyombo vya habari kuhusu kesi za Kenya;
  • Kampeni isiokuwa ya kawaida kwa  vyombo vya habari kijamii kwa kufichua utambulisho wa mashahidi waliopewa ulinzi katika kesi ya Kenya;
  • Jitihada nyingi zilizofanywa kwa pamoja kwa kunyanyasa, kuwatisha na kutishia watu ambao wanataka kuwa mashahidi.

Kwa uhakika, kushindwa kwa Serikali ya Kenya kutoa kwa Ofisi yangu ushahidi wa vipengele muhimu imekuwa na madhara makubwa mabaya katika kesi hii. Imewanyima waathiriwa katika kesi hii kujua kwa ukamilifu kilichotendeka mnamo 2007-2008. Pia imedhoofisha uwezo wangu wa kufanya uchunguzi kamili. Mwishowe, imezuia Majaji wasitekeleze majukumu yao muhimu ya kutathmini ushahidi na kutafuta ukweli.

Hatimaye vikwazo ambazo tumevipata kwa kujaribu kupata ushirikiano unaohitajika kwa uchunguzi huu kwa sehemu kubwa, pamoja na kwa mfululizo, imechelewesha na kuzuia mkondo wa sheria kwa waathiriwa katika kesi hii. 

Chanzo: Ofisi ya Mwendesha Mashtaka

Source : Office of the Prosecutor