Video na Sauti (Kwa Kiingeraza)
YouTube (kwa kutazama)
Video (MPEG-4) kwa kushusha
Sauti (MPEG-3) kwa kushusha
Jana,
idadi kubwa wa Majaji wa Chumba cha kesi V (A) wa Mahakama ya Kimataifa
ya Jinai ("ICC" ama "Mahakama"), iliondoa mashtaka dhidi ya Bwana
William Samoei Ruto na Bwana Joshua Arap Sang.
Chumba ilikataa
kumwachia mshtakiwa kutokana na hali maalum ya kesi hii. Kwa kufanya
hivyo, Chumba iliunga mkono msimamo wa upande wa Mashtaka ya kuwa kesi
hii imedhoofishwa na washahidi kuingiliwa, na kisiasa ya utaratibu wa
kisheria. Uamuzi ulibanisha zaidi kuwa ushahidi mwingine ingeweza
kupatikana kwa upande wa Mashtaka "kama ingekuwa na uwezo wa kushtaki
kesi katika hali tofauti, bila uadui kuelekezwa kwenye upande wa
Mwendesha Mashtaka, washahidi wake na Mahakama kwa jumla."
Chumba
ilisema wazi kwamba uamuzi wao ni bila ya kuathiri dhulma ya kutokuwa na
hatia au upande wa Mashtaka kuleta kesi kwa msingi ya madai sawa katika
siku zijazo, au kwa namna tofauti, katika mwanga wa ushahidi mpya.
Tunasikitika
kwamba kutokana na juhudi za makusudi na za pamoja ili kufuta kesi hii
kwa njia ya washahidi kuingiliwa, Majaji wamezuiwa kutoka kuamua hatia
au kutokuwa na hatia ya Washtakiwa juu ya uhalali kamili ya kesi. Jambo
pia ya kusumbua ni kwamba mashambulizi dhidi ya kesi hii ina - kwa sasa -
imekanusha waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-2008
nchini Kenya haki yao kama walivyo stahili.
Kwa hivi sasa tuko katika mchakato wa makini kutathmini uamuzi wa Chumba cha kesi na kuamua hatua sahihi za kufuata.
Ukweli
ni kwamba Mashtaka mbele ya ICC inaweza simama ama anguka kulingana na
kujitokeza kwa washahidi na kusema hadithi yao mbele kwa chumba cha
mahakama.
Katika kesi hii, washahidi 17 waliokuwa wamekubali
kutoa ushahidi dhidi ya Washtakiwa hatimaye walijiondoa katika
ushirikiano yao na Mahakama.
Washahidi wa upande wa Mwendesha
Mashtaka walitishwa, wakatengwa kijamii na kuhatarishwa ili wasitoe
ushahidi. Mwishowe, Chumba cha kesi walikuwa katika athari kuzuiwa
kutoka kuwa na nafasi ya kupima uhalali kweli ya kesi ya upande wa
Mashtaka.
Imekuwa safari ngumu, tangu Ofisi ya Mwendesha Mashtaka
ilifungua uchunguzi ya ghasia baada ya uchaguzi namo 2007-2008 nchini
Kenya namo Machi 2010. Moja ya lengo letu thabiti, daima imekuwa kupata
haki huru na bila ya upendeleo kwa waathiriwa wengi wa ghasia hilo.
Ghasia
yaliyoenea nchini Kenya baada ya uchaguzi namo Desemba 2007 ilikuwa ya
kushangaza kwa watu wote. Majirani walichukua silaha dhidi ya majirani;
Wanakenya waligeuka juu ya Wanakenya wenzao; wanaume, wanawake na watoto
walichomwa hai, ubakaji au kukatwakatwa hadi kufa. Wanakenya zaidi ya
elfu waliuawa; maelfu zaidi walijeruhiwa; na watu zaidi ya mia mbili
elfu walikimbia nyumba zao.
Kwa mujibu wa mamlaka yetu chini ya
Mkataba wa Roma, tuliamua kuanzisha uchunguzi wa ghasia za baada ya
uchaguzi tu wakati ilikuwa wazi kuwa waathiriwa wa unyanyasaji hilo
hawakuwa na namna lolote wa sheria katika nchini Kenya na maombi yao kwa
uwajibikaji ilianguka kwenye masikio ya viziwi.
Ofisi hii
ilishiriki katika juhudi kanuni na bidii, kutoka Februari 2008 mpaka
Novemba 2009, kuhimiza mamlaka ya Kenya itumize wajibu wao chini ya
Mkataba wa Roma wa kuchunguza na kushtaki wale walioendesha na kuchochea
ghasia namo mwaka wa 2007-2008. Ingawa Serikali ya Kenya ilikubali
kuanzisha Mahakama Maalum ifikapo Novemba 2009, tarehe hiyo ilifika na
ikamalizika. Pamoja na kuongeza uharaka, Wanakenya kutoka kila matembezi
ya maisha walitoa wito kwa ICC itekeleze mamlaka yake.
ICC
iliingilia kati ya Kenya wakati ilionekana wazi kwamba Mahakama Maalum
haitaanzishwa. Pamoja na hayo, mabadiliko ilipoingia katika Katiba mpya
ya Kenya namo 2010, Serikali ya Kenya ilionekana kuwa hawawezi kushika
watu binafsi kutoka nchini Kenya, tabaka la wanasiasa wenye uwezo
kuwajibika kwa kutegemea nguvu ili kufikia malengo ya kisiasa.
Mkataba
wa Roma wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai imefafanua kazi yangu:
kupambana na ukatili kwa makosa makubwa zaidi ya wasiwasi na jumuiya ya
kimataifa, kwa kuchunguza na kufungulia mashtaka ya uhalifu - kitaalum,
kwa haki, na bila uwoga au upendeleo.
Ofisi yangu inafanya kila
kitu ndani ya uwezo wake kuhakikisha kwamba wale ambao waliusika kwa
uhalifu ndani ya mamlaka ya Mahakama wanaletwa kwa haki. Kama Mwendesha
Mashtaka, mimi binafsi nina nia ya kuhakikisha kwamba ofisi hii
inazingatia viwango vya juu vya uadilifu, taaluma, na ufanisi katika
kutimiza mamlaka yake.
Mkataba wa Roma inahitaji Ofisi yangu
kutumia mamlaka yake ya kuthibitisha ukweli. Katika kesi hii, tulijaribu
kutambua, kuhakikisha, na kuweka mbele ya Majaji, ushahidi ambao
unaweza kuwasaidia kuamua iwapo Washtakiwa walihusika na vurugu ambayo
ilitokea upande wa Bonde la Ufa nchini Kenya kufuatia uchaguzi mwaka wa
2007.
Hata hivyo, licha azimio letu la kufunua ukweli na
kuendeleza kozi ya haki nchini Kenya, kesi hii iliharibiwa hatimaye na
'dhoruba kamili' ya mashahidi kuingiliwa na siasa kali kuwekwa kwa
Mahakama na mamlaka ya kisheria na kazi yake.
Kulikuwa na kampeni
kali ya kutambua watu ambao wangeweza kutumika kama washahidi kwa
upande wa Mashtaka katika kesi hii na kuhakikisha kwamba hawakutoa
ushahidi. Mradi huu wa vitisho ulianza kabla ya kuanza kwa uchunguzi
wetu katika nchini Kenya, na ikazidi katika wiki ya mwanzo wa kesi, na
kuendelea katika maisha ya kesi. Matokeo ni kwamba, mashahidi
walituambia kwamba waliogopa mno kujitoa kwa kushuhudia dhidi ya
Mshtakiwa. Wengine, ambao awali walitupa akaunti ya kile walichokiona
katika kipindi baada ya uchaguzi, hatimaye walibadilisha ushahidi wao,
na wakakataa kuendelea kushirikiana na Mahakama.
Zaidi ya hayo,
katika mikutano ya hadhara ya maombi, wanasiasa nchini na viongozi wa
jamii waliwatambua mashahidi wa Mwendesha Mashtaka kama waongo na wote
walikuwa wametoa ushahidi wa uongo. Kwa vyombo vya habari ya kijamii,
bloggers bila majina walishiriki katika mkondo wa kutosha wa uvumi
kuhusu utambulisho wa mashahidi walio na ulinzi. Uvumi huu mara nyingi
ulisababisha ufafanuzi uchungu kuhusu nia ya mashahidi kwa kushirikiana
na Mahakama.
Hii, basi, ni ukweli mkali kwamba mashahidi, na
wakati mwingine familia zao, walikabiliwa katika kesi hii. Mashahidi,
hata hivyo, lazima tuwatie moyo kwa jukumu wao muhimu wanayofanya katika
uamuzi wa Majaji ya ukweli, na kuheshimiwa kwa ujasiri wao. Hakuna
shahidi anastahili kukabili na hali ile hawa mashahidi walikabiliana
nayo katika kesi hii.
Ndani ya mamlaka na uwezo wetu, tulitafuta
kukabiliana na kuingiliwa na utawala wa haki katika kesi hii, kwa
kuchunguza matukio ya vitisho kwa shahidi au rushwa, tuliweka kumbukumbu
ushahidi, na kuzingatia Chumba cha hali kama vilivyotokea. Tulipata kwa
Majaji hatua zaidi za kukinga mashahidi. Kufuatia uchunguzi wetu,
tulitafuta na tukapata vibali vya kukamatwa kwa Mabwana Walter Osapiri
Barasa, Paul Gicheru na Phillip Kipkoech Bett, juu ya madai ya kuzuia
mwendo wa haki.
Kama ilivyoelezwa katika uamuzi wa jana,
Washtakiwa, Bwana Ruto na Sang walifaidika kutokana na kuingiliwa huo
kwa utawala wa haki.
Hamna kwa watuhumiwa hao watatu, ambao
wameshtakiwa na Mahakama kwa kuzuia mwendo wa haki katika kesi hii, bado
hawaja salimishwa kwa Mahakama na Serikali ya Kenya.
Natoa wito
kwa mamlaka ya Jamhuri ya Kenya itimize majukumu yao chini ya Mkataba ya
Roma, na kusalimisha watuhumiwa hawa watatu kwa Mahakama bila kuchelewa
zaidi, ndivyo hatia yao au kutokuwa na hatia ya mashtaka dhidi yao
iweze kutegemewa na bila upendeleo iuamuliwe katika kesi.
Kuingilia
mashahidi na mazingira ya uhasama inatazamwa katika uamuzi wa jana
inasisitiza umuhimu wa Serikali ya Kenya kutekeleza majukumu yake na
kujisalimisha watuhumiwa hao mikononi mwa Mahakama.
Pia,
tulitafuta na tulitaka kutumia hatua ya ubunifu wa kisheria wa kuhifadhi
ushahidi yenye tulikuwa tumekusanya. Wakati washahidi muhimu
walibadilisha akaunti zao za matukio, tulitafuta msaada wa Chumba cha
kesi kuwalazimisha kutokea mbele ya Majaji, ili matoleo yao inayo
pingana iweze kujaribiwa mbele ya Chumba. Wakati tulikuwa tumekusanya
ushahidi wa kutosha kuonyesha ya kwamba mashahidi walikuwa wakikana
akaunti zao za awali, kwa sababu ya kuingiliwa, tuliomba Chumba cha kesi
ikubali ushahidi wa kwanza wa mashahidi kulingana na marekebisho ya
Ibara 68 ya uwezo wa kisheria wa Mahakama.
Hata hivyo, namo
tarehe 12 Februari 2016, Chumba cha Rufaa iliamua kubadilisha uamuzi wa
Chumba cha kesi na kukubali kuweka katika rekodi ya kesi hii ya awali,
ushahidi ya lawama wa mashahidi ambaye walikuwa wameingiliwa. Hasa,
ingawa Chumba cha Rufaa iliamua kwamba hatungeweza kutumia marekebisho
ya Ibara 68 kwa mambo ya zamani iwe ushahidi wa mashahidi
waliobadilisha msimamo yao, haiku badilisha hitimisho la Chumba cha kesi
ya kwamba kulikuwa na utaratibu kuingilia mashahidi katika kesi hii.
Ni
thamani kusisitiza hatua hiyo, licha ya taarifa potofu na kutokuelewana
yalionekana katika vyombo vya habari ya kijamii na za jadi, hii haikuwa
kesi ambayo yalilenga nchi au jamii fulani ndani ya nchi. Vile vile, ni
lazima kamwe tusisahau kwamba mamia ya waathiriwa wa Kenya walishiriki
katika kesi hii.
Ningependa kusisitiza hatua hii. Hii haikuwa
kesi kuhusu uwajibikaji wa pamoja wa Wakalenjin, Wakikuyu, Wakisii,
Wajaluo, Wamaasai ama wananchi wa Kenya. Hii ilikuwa kesi ya mtu binafsi
kuwa na kujibu kwa mashtaka ya jinai ilioletwa dhidi yake katika uwezo
wake binafsi na ambaye ana hatia au hana mara kuangaliwa katika kesi ya
haki na bila ya upendeleo.
Katika mwendo wa kawaida wa matukio,
Serikali ya Kenya ingekuwa mshirika wa Ofisi hii, kwa sababu kesi
ilikuwa inahusu uhalifu dhidi ya Wanakenya, uhalifu inavyoelezwa na
uliowekwa kwa mkataba na kuridhiwa na Serikali ya Kenya. Kama nchi
inayounda Mkataba wa Roma, Serikali ya Kenya ina wajibu za kimataifa na
za katiba kusaidia Ofisi katika uchunguzi wetu.
Hata hivyo, licha
ya kuhakikishiwa mara kwa mara ya ushirikiano na Mahakama, Serikali ya
Kenya ilichagua msaada wa kutoa kwa upande wa Mashtaka. Matokeo halisi
ni kwamba Ofisi yangu haikuwa na huduma kamili ya nyaraka na kumbukumbu
ambayo ingeweza kuwa na ushahidi wa thamani au kuweza kumwaga mwanga
katika ukweli.
Hatimaye, vikwazo zilizotokea katika juhudi zetu
za kuchunguza na kufungua mashtaka kuwa ngumu na kuchanganyikiwa
kutokana na mwendo wa haki kwa waathiriwa katika kesi hii, na hii ni
lazima suala la masikitiko makubwa.
Tunajifunza kutoka vikwazo
zetu. Ofisi hii ina nia ya kupitia upya, kurekebisha na kuboresha mbinu
zake za kazi. Hakika, tangu niwe Mwendesha Mashtakwa mwaka 2012,
tumetekeleza mfululizo wa mabadiliko ili kuongeza ufanisi wa kazi yetu,
juu ya mambo ambaye tumejifunza. Mipango mikakati ya hivi karibuni ni
mfano mmoja tu wa juhudi hizo saruji, ambayo tayari kuzaa matunda katika
mazoezi.
Nataka kuchukua fursa hii kuwashukuru wale wote ambao
walisaidia Ofisi hii kwa kazi yake nchini Kenya, kwanza kabisa,
waathiriwa wenyewe.
Nawashukuru mashahidi katika kesi hii, ambao
walikuja kwa ujasiri na ushahidi kwa gharama kubwa binafsi. Nawashukuru
jamii maalum ya Wakenya - wakulima, madaktari, waandishi wa habari,
wafanyi kazi wa misaada na wengine- ambao kutoka mwanzo inaweza kuwa
hawakutaka kutumika kama mashahidi katika kesi hii, lakini hata hivyo
walitoa ufahamu muhimu katika kile kilichotokea katika kipindi hicho cha
vurugu baada ya uchaguzi.
Hakika, napenda kuwashukuru wale
wote, ndani na nje ya Kenya, ambao uhodari na ushupavu na bila kuchoka
kuwezesha na kusaidia kazi yetu katika nchini Kenya kwa sababu ya hatia
yao na kujitolea kwao sababu ya haki. Hatimaye, napenda kuwashukuru
Mataifa Wanachama wa Mkataba wa Roma wale ambao walilishirikiana na
Ofisi katika mahusiano ya kesi hii na kwa imara walisimama na kanuni
yanazingatiwa katika Mkataba wa Roma.
Wakati wa mwendo wa kesi
hii, nimeguswa undani na wanyonge na ajabu ujasiri, imani na uvumilivu
wa watu wengi wa Kenya ambaye tuliwasiliana nao.
Uamuzi wa jana
ina ujumbe nguvu: Kuingilia mashahidi na kupotosha chanzo cha haki
hautavumiliwa katika mahakama ya ICC. Muda iko upande wa haki.
Licha
ya hayo matatizo Ofisi yangu imepata kwa kesi hii, tutabaki imara
katika kutekeleza azma yetu ya haki ya kimataifa ya uhalifu.